Mkali wa Bongo fleva nchini, Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari the Boss Lady wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume baada ya Zari kujifungua salama katika hospitali ya Netcare jijini Pretoria nchini Afrika Kusini leo.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Diamond kupitia ujumbe aliouandika kwenye akaunti yake ya Instagram ameeleza kuwa mtoto wao huyo amezaliwa majira ya saa 8:35 usiku kwa saa za Afrika kusini ambazo ni sawa na saa 10:35 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagrama Diamond ameandika Zari amejifungua leo saa 10:35 alfajiri katika hospitali ya Netcare  Pretoria South Africa.

Kwa upande wa Diamond huyo anakuwa mtoto wa pili kwa mpenzi wake  huyo lakini lkwa upande wa Zary huyo anakuwa mtoto wa tano.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *