Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz anatarajia kutumbuiza kwenye kilele cha maadhimisho ya mbio za Mwenge zitakazofanyika katika uwanja wa Amani visiwani Zanzibar Oktoba 14 mwaka huu.

Taarifa hiyo imethibitishwa na mkuu wa mkoa wa mkoa Mjini Magharibi, Ayoub Mohmoud ambako ndipo kutafanyika kilele cha maadhimisho ya mbio za mwenge kitaifa.

Diamond Platnumz na kundi lake la WCB wamethibitisha kuwa watatumbuiza siku hiyo ya tarehe 14/10/2017 visiwani Zanzibar.

Kupitia akaunti yake ya Instagram mkuu wa mkoa huyo ameandika kuwa  #icantwait Nikiwa Kama Mkuu wa Mkoa Wa Mjini #zanzibar napenda kukukaribisha wewe mdogo wangu @diamondplatnumz pamoja na team Yako nzima katika siku ya tarehe 14/10/2017 Katika viwanja vya amani!. Ni matarajio yangu wana mkoa wa mjini magharibi wanakusubiri kwa hamu!. Confirmed diamond platinum live performance at Amani Stadium!. #kilelechamwengezanzibar #MiminaWewe #karibuninyote.

Mwenge wa Uhuru utaihitimisha shughuli zake Oktoba 14 mwaka huu baada ya kuzunguka mikoa yota nchini ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *