Staa wa Bongo fleva, Diamond Platnumz amethibitisha kuwa yupo kwenye mipango ya kuongeza nguvu kwenye lebo yake ya WCB kwa kumsaini msanii wa nje ya Tanzania.

Diamond amesema hayo wakati akijibu swali la shabiki kwenye mtandao wa Twitter, lililokuwa linauliza “WCB hamjafikiria kusaini msanii nje ya Tanzania au mtafanya?”

Staa huyo alijibu swali hilo kwa kuandika, “Soon.” kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter kutokana na swali hilo alilouliza mshabiki huyu.

Lebo ya WCB kwasasa ianmiliki wasanii watatu ambao ni Hamonize, Raymond na Rich Mavoko ambao wanaonekana kufanya vizuri katika anga ya muziki wa Bongo fleva kutokana na nyimbo zao kukubalika na mashabiki.

Diamond kwasasa anataka kutanua lebo yake hiyo kwa ajili ya kuongeza mashabiki ambapo kwasasa anataka kuongeza msanii mwingine katika lebo lakini akaweka wazi huyo msanii atakuwa wa nchi gani.

Diamond ni msanii mkubwa kwasasa barani barani Afrika ambapo amefanya collabo nyingi na wasanii wa nje ya nchini mpaka kupelekea kupata tuzo ya MTV pamoja na tuzo za AFRIMA zinazotolewa nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *