Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema wimbo mpya upo njiani kwani mapokezi ya nyimbo zake mbili Yatapita na Zuwena yamemshangaza.

Yatapita kupitia mtandao wa YouTube imeangaliwa mara Milioni 8. 3 huku Zuwena ikiangaliwa mara Milioni 5 ndani ya siku tano.

Baada ya mapokezi hayo mazuri, muimbaji huyo ambaye alitangaza balaa mwaka huu ametoa taarifa hii .

“Inahitaji Nguvu, Baraka, Upendo mkubwa na Sapport kubwa toka kwa watu, Kutoa wimbo na kukaa siku tatu haujapost chochote kwenye Page yako mbele,

No Machallenge wala chochote mbele kupush wimbo, Halaf kila siku wimbo ukazidi kuendelea kufanya Vyema.

Hakika Mashabiki zangu mnanipa faraja, nyinyi ni zaidi ya Mashabiki kwangu, Nyinyi ni Familia Yangu, na Nawashkuru kwa kila Support, Upendo na jema mlitendalo kwangu Vyote Naviona na Niwaambie Huu Mwaka Ni vyuma juu ya Nondo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *