Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka na kutangaza tarehe rasmi ya kuachia EP yake ya kwanza ambayo ameipa jina la FOA.

Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha kuwa tarehe 11 Machi mwaka huu ndio itakuwa siku rasmi ya kuachia EP yake ya kwanza toka aanze muziki hapa nchini.

Pia Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram (Story) Amepost Ufunguo Wa Gari Yake Ya Thamani Rolls Royce Iliyokuwa na Rangi Ya Orange Akisema Kuwa Ina Aina Ya Foa Ndani Yake.

Mwanamuziki huyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kuipokea EP yake hiyo kwani nyimbo zilizomo kwenye EP hiyo ni kali na kila shabiki wake ata enjoy muziki mzuri kutoka kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *