Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnum ameizindua rasmi perfume yake ya Chibu Perfume kwenye Mall ya GSM Pugu Road Dar es salaam.
Diamond amesema Perfume hiyo asili yake ni Dubai kwa sababu inaaminika kuwa Dubai ndio sehemu kunakotoka manukato mazuri.
Kwa Upande wake Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam amesema perfume hiyo itauzwa kwa Tsh 105,000 kwa bei rejareja.
Mwanamuziki huyo ameingia kwenye ujasiliamali baada ya kuzindua perfume hiyo leo katika ukumbi wa GSM Mall jijini Dar es Salaam.