Staa wa Bongo fleva, Diamond Platnumz ametoa msaada wa Milioni 20 kwa taasisi ya “GSM Foundation” ili kusaidia huduma ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi nchini.

Diamond ameonyesha kuguswa na matatizo hayo yanayowakabili watoto pamoja na jitihada za taasisi hiyo na kuamua kuchangia kiasi hicho cha fedha ili kiweze kusaidia na kufanikisha tatizo hilo.

Upasuaji

Madaktari bingwa kutoka MOI wakishirikiana na taasisi ya GSM Foundation imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali ya hapa nchini ili kutoa huduma hiyo bila gharama yoyote kwa upasuaji huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond aliandika “Moyo wangu unaniambia nisingeshikwa mkono ama kusaidiwa na watu basi nami nisingeweza leo hii kufikia hatua hii ndogo niliofikia na ndio maana kidogo nikipatacho huwa napenda kusaidia wenzangu,

Baada ya kutoa mchango huyo kwa upande wa GSM Foundation, kupitia ukurasa wao wameandika “Leo tumepokea hundi ya shilingi milioni ishirini (20,000,000/=) kutoka kwa @diamondplatnumz kama mchango wake kwa #GSMFoundation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *