Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amethibitisha kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga yatakayofanyika kesho nchini Uganda.

Diamond amethibitisha hayo mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya alipokwenda kwa ajili ya shoo ya Koroga nchini humo na kuthibitisha kuhudhuria mazishi hayo nchini Uganda.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa atahudhuria mazishi hayo kwa ajili ya kumfariji mpenzi wake Zari ambaye alikuwa mume wa Ivan ambapo wamefanikiwa kupata watoto watatu ambao wote wa kiume.

Diamond amesema kuwa ameongea na Zari kama atahudhuria mazishi hayo baada ya kumaliza shoo yake ya Nairobi.

Ivan Ssemwanga maarufu kama The Don amefariki Alhamisi iliyopita nchini Afrika Kusini baada ya kulazwa hospitali kutokana na kuugua ugonjwa wa shambulio la moyo.

Mwili wa Ivan umewasili jana nchini Uganda kutokea Afrika Kusini kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *