Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea hospitali ya Amana.

Akiwa hospitali hapo, Diamond ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh4 milioni pamoja na baadhi ya vitu kwa wagonjwa.

Diamond ambaye sasa anatamba na ngoma yake ya Hallelujah, amesema alifikia uamuzi wa kwenda kwenye hospitali hiyo kwa kuwa ndiyo mahali alipozaliwa.

Amesema anajivunia kuwa na watu wazuri wa karibu ambao wanamshauri kurudisha kwenye jamii inayomzunguka.

Kwa upande wake, Kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Shaany Mwaruka amempongeza Diamond kwa uamuzi huo na kutaka watu wengine waige mfano huo.

Dk Mwaruka amesema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba kutokana na idadi kubwa ya watu wanaowahudumia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *