Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz licha kuahidi kuwa Mwaka huu 2023 atafanya maajabu katika Muziki wake kwa kuachia nyimbo tofauti tofauti.

Pia Diamond Platnumz ameweka wazi swala lingine analolitamani kwa Mwaka huu 2023 kuwa anahitaji kuongeza Mtoto Mwingine.

Mpaka sasa Staa huyo anawatoto Wanne ambao, Tiffa, Nillan Dylan na Naseeb Junior ambao amezaa na wanawake watatu tofauti.

Wanawake hao ni Zali ambae amezaa nae Watoto wawili, Hamisa Mobetto aliyezaa nae mtoto mmoja na Tanasha nae amezaa nae mtoto mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *