Mkali wa Bongo fleva, Diamond Platnumz amepiga show ya kufa mtu kwenye tamasha la Sand Music lililofanyika katika fukwe za Living stone nchini Malawi jana jumamosi.
Tamasha hilo limehudhuriwa na watu kibao kutoka ndani na nje ya Malawi na kusababisha watu kufurika kwa wingi kwenye tamasha hilo mashuhuri nchini Malawi licha ya mvua kubwa kunyesha lakini show iliendelea kama kawaida.
Diamond anaonesha kuiteka sana Afrika kutokana na show zake anazofanya kujaza watu wengi ambao wameonesha kumkubali sana mwanamuziki huyo kutoka nchini Tanzania.
Mwezi uliopita Diamond alifanya show katika mji a Mombasa nchini Kenya na watu warifurika kwenye show hiyo.
Kutokana na show hizo kujaza watu wengi inaonekana kabisa Diamond ni mwanamuziki anayeongoza kwa kujaza watu wengi kwenye show zake kuliko mwanamuziki yeyoto nchini Tanzania kwasasa.