Diamond Platnumz ameamua kuingia mkataba na kampuni ya kimataifa Universal Music Group (UMG) ili iweze kumsapoti kusambaza nyimbo zake.

Ni dili ambayo thamani yake kwa mujibu wa lebo ya WCB, imewatunishia mifuko kwa faida inayofikia bilioni 2 na zaidi lakini je, mashabiki wa Bongo wataweza kuendana na mfumo wa Universal Music Group?

Hata wiki haijafika, wale wazee wa ‘kuteleza tu…….’ Wazee wa kuchukua LINK YouTube na kupakua mizigo bila kuchangia gharama ‘wameanza vilio’.

Mkataba wa Diamond na Universal Music Group pamoja na mambo mengine pia unahusisha kampuni hiyo kusimamia mauzo yote ya kazi za Diamond Platnumz na ukusanyaji wa mirabaha kwenye baadhi ya maeneo.

Hivyo kwa sasa watanzania wanapaswa kuishi kwa mfumo wa uendeshwaji wa kampuni ya UMG, namna wanavyosambaza kazi hizo na kuziuza.

Huenda Diamond Platnumz akapoteza mashabiki wengi Afrika Mashariki kutokana na mfumo huo mpya wa usambazaji wa kazi zake ingawa hili linaweza kuonekana baada ya miaka kadhaa.

Ukitaka nyimbo za Diamond Platnumz kwa sasa hii ndio mitandao utakapozipata.

screen-shot-2017-02-03-at-15-39-52

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *