Leo ni siku ya kuzaliwa Zari the boss lady ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnmuz.

Diamond akubaki nyuma kumpongeza mpenzi wake huyo kwenye siku yake hiyo ya kuzaliwa.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Diamond ameandika maneno mazuri ya kumsifia mpenzi wake huku akisema kuwa mwanamke huyo anamchango mkubwa sana kwenye mafanikio yake aliyonayo.

Diamond ameanza kwa kuandika “Uzuri na Urembo pengine ningetembea nikakuta baadhi wanao pia… Lakini Akili, Hekma, pamoja na Roho yako ya kwenye Shida na Raha kwangu ndio kitu pekee kinachonifanya nikupende na kukuthamini zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda”

Pia ameongeza kwa kuandika kuwa wanaposema kwenye kila Mafanikio ya Mwanaume kuna Mwanamke imara nyuma, hawamaanishi eti anaepika na kuosha vyombo sana ama kufua nguo kila siku… Hapana! ni mwanamke Mwenyekuwa bega kwa bega na Mpenzie kwenye Shida na Raha… Happy birthday General”.

Diamond na Zari mpaka sasa wamefankiwa kupata watoto ambao ni wake na kiume aliyezaliwa mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *