Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz leo amemtambulisha msanii mpya wa WCB anayeitwa Lavalava.

Diamond amemtambulisha msanii huyo kupitia kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na kituo cha radio cha Clouds Fm.

Katika utambulisho huo msanii huyo pia ameachia wimbo wake kwa mara ya kwanza inayoitwa kwa jina la ‘Tuachane”.

Diamond amesisitiza kuwa anawajibika kuwasaidia wengine kwa kuwa hata yeye amesaidiwa ndiyo maana amefikia hatua hiyo hivyo anapenda na wengine wakifikia mafanikio kama yake kwa kuwasaidia.

Diamond amewashukuru sana Clouds Media kuwa kama daraja kuwasaidia wengine kwenye maisha ya binadamu.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Kama mimi nilisaidiwa ni nafasi yangu kuwaunga mkono kuwasaidia wengine walio katika matatizo.

Diamond amesema kuwa huu ni msimu wa shukrani na yeye amemshukuru kila mtu na nawashukuru sana Clouds FM kwa sababu wamenisaidia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *