Baada ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kuachia wimbo mpya ‘Eneka’ staa kutoka Nigeria, Yemi Alade ameonyesha kuguswa na kibao hiko.

Kwenye wimbo huo Diamond amesikika akiimba maneno ya lugha ya Igbo inayopatikana nchini Nigeria.

Kupitia akaunti ya Instagram ya Diamond ambapo ameposti video hiyo mpya, Yemi Alade amecoment kwa kumsifai Diamond kuimba lugha hiyo ya Nigeria.

 Eneka ni moja kati ya nyimbo ambazo Diamond ameziachia kwa kushtukiza na mapokezi yake yameonekana kuwa makubwa tofauti na alivyotarajia.

Kitendo cha Diamond kutumia baadhi ya maneno ya lugha ya nchini Nigeria ndio kimeonekana kumfanya Yemi kuupenda zaidi wimbo huo.

Kupitia Instagram Yemi Alade amecont kama ifuatavyo. “Omg !you are singing in IGBO @diamondplatnumz,” .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *