Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka sababu ya kuweka picha ya Alikiba katika ofisi yake ya WCB.

Diamond amesema kuwa ameamua kuweka picha za Alikiba katika ofisi yake kwasababu mwanamuziki huyo ana mchango mkubwa na muziki wa Bongo Fleva hadi ulipofika kwasasa.

Muimbaji huyo ameweka picha ya kila msanii ambaye ana mchango mkubwa katika kukuza muziki wa Bongo Flava katika ofisi za studio yake ya WCB.

Diamond ameendelea kusema kuwa angekuwa mnafiki kama asingeweka picha ya Alikiba kwasababu ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Pia amesema kuwa ofisi ya WCB si yake wala msanii wa WCB bali ni Bongo Fleva kwa hiyo kila mmoja ana staili kuwemo ndani ya familia ya WCB.

Ameongeza kuwa watu wanaohoji au kushangaa kitu hicho ni hisia tu na kila mtu anapaswa kuwa na hisia zake lakini haikuwa hivyo kama wanavyofikiria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *