Staa wa Bongo fleva, Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka sababu zilizomfanya anunue nyumba nchini Afrika Kusini.

Staa huyo amesema sababu iliyomfanya anunue nyumba nchini humo ni yeye mwenyewe kupata urahisi wa makazi pindi anapokwenda Afrika kusini kwa ajili ya kazi zake za muziki pamoja na familia yake ambayo muda mwingi inaishi huko.

diamond-platnumz823-710x710

Diamond amesema kingine kilichomsukuma kununua nyumba huko ni kwasababu ya mtoto wake Tiffah pamoja na mtoto wake mwingine ambaye anatarajiwa kuzaliwa hivi karibuni baada ya mpenzi wake Zari kuwa na ujauzito.

Pia staa huyo amesema kingine kilichomfanya anunue nyumba nchini Afrika Kusini ni kwasababu amechoka kuhangaika mahotelini kwa ajili ya malazi pindi akiwa nchini humo pamoja na familia yake kwa ujumla.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *