Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz amefanya video mpya ya wimbo wake na mkali wa hip hop kutoka Pande za Marekani, Rick Ross.

Mameneja wa mwanamuziki huyo, Babu Tale na Sallam wamekuwa wa kwanza kuweka picha na vipande vya video ambavyo vinaonesha wawili hao wakishuti video hiyo katika jiji la Miami nchini Marekani.

Msanii wa WCB, Ray Vanny ameonekana katika baadhi ya picha akiwa na Diamond na Rick Ross. Ray aliambatana na Baba Tiffah nchini Marekani kwenye tuzo za Afrimma.

Diamond ambaye alikuwa nchini Marekani mapema mwezi huu kwa ajili ya kushiriki tuzo za Afrimma, ametumia nafasi hiyo kumaliza kazi hiyo na Rick Ross ambaye ni balozi mwenzake wa kinywaji cha Luc Belaire.

Wimbo huu wa Diamond utakuwa wapili kimataifa baada ya kufanya ngoma na mwanamuziki Neyo kutoka Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *