Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnum amefunguka jinsi ya kununua nyimbo kwenye mtandao wake wa Wasafi.com aliouzindua jana.

Diamond amesema kuwa mtandao huo wa kuuza nyimbo upo tofauti sana  na mitandao mingine ktokana na uuzaji wake.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa ‘Wasafi.Com inamuwezesha mtu kununua nyimbo kwa kutumia kadi za benki, pia wasafi.com ukiingia haihitaji kulog in kama vile facebook na vitu kama hivyo, we unaingia unanunua nyimbo yako unatulia zako’.

Diamond ameingia kwenye upinzani na mitandao mingine ya uuzaji wa nyimbo kama vile  Mkito, Africasongs na nyinginezo.

Kwenye uzinduzi wa mtandao huo wa Wasafi.com ulihudhuriwa na wasanii tofauti wa Bongo Fleva kama vile, Cassim Mganga, Ben Pol, Chege, Temba na Barnaba na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *