Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz anadaiwa milioni 400 na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Hayo yamesemwa na mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia Bungeni wakati wa mjadala wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Mbunge huyo amesema kuwa wilaya ya Kinondoni ina wasanii wengi maarufu na wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi kutokana mauzo ya kazi yao.

Mtulia amesema kuwa Diamond amemwambia anadaiwa na TRA milioni 400 kutokana na malimbikizi ya kodi.

Mbunge huyo ameshauri kuwa kutokana na wasanii kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na kazi zao za Sanaa, ameiomba serika kuimarisha mapambano dhidi ya wizi wa kazi za sanaa nchini na siyo kutulia mkazo kwenye suala la kodi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *