Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anatarajia kupanda kizimbana leo kwa madai ya kesi ya uchochezi dhidi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Ijumaa wiki iliyopita Lema alipelekwa gereza la Kisongo Arusha kutokana na kunyimwa dhamana katika kesi nyingine ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya rais Magufuli hatua ambayo imepingwa na chama chake na wakili wake.

Hata hivyo Chadema kinatarajia kuwasilisha maombi mahakama kuu kuomba mbunge huyo Lema apewe dhamana.

Katibu mkuu wa Chadema mkoa wa Arusha, Calist Lazaro amesema kuwa hawakuridhishwa na pingamizi la dhamana liliowekwa na mawakili wa serikali wiki iliyopita kwasababu Lema alikuwa tayari amepewa dhamana na Hakimu.

Naye Wakili Shaki Mfinanga amesema kuwa leo watawasilisha maombi ya dhamana ya Lema wakiwa na mawakili wa Chadema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *