Wachezaji watatu wa klabu ya Yanga, Deus Kaseke, Simon Msuva na Obrey Chirwa wamesimamishwa kucheza mechi za Ligi Kuu msimu ujao baada ya kumsukuma na kumwangusha Mwamuzi, Ludovic Charles katika mchezo huo dhidi ya Mbao FC.

Adhabu hiyo imetolewa leo  na kamati ya Saa 72 baada ya kupitia tukio hilo lililotokea mechi ya mwisho kati ya Yanga na Mbao FC iliyofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Wachezaji hao wamepewa adhabu hiyo huku suala lao linatarajiwa kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa upande mwingine, Yanga imepigwa faini ya shilingi milioni 5 kwa makosa waliyofanya katika mechi mbalimbali katika ligi kuu Tanzania Bara msimu ulioisha.

Adhabu hiyo ni sehemu ya uamuzi wa adhabu mbalimbali kutoka Kamati y Saa 72 uliotangazwa leo baada ya kupitia michezo mbalimbali za ligi hiyo ambapo kwa upande wa Yanga umezingatia kuwa klabu hiyo imekuwa ikirudia rudia baadhi ya makosa hasa kosa la kutoingia katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kupita mlango usio rasmi katika mechi hiyo iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Pia Yanga imepigwa faini ya sh. 1,500,000 (milioni moja na laki tano) kwa kutoingia vyumbani na faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuonyesha vitendo vinavyoashiria ushirikiana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *