Kiungo mkabaji wa Yanga, Deus Kaseke jana amefanya mazoezi na timu hiyo baada ya kukosekana kwa wiki tatu kutokana na maumivu aliyopata baada ya ajali ya pikipiki.

Kiungo huyo alikosekana ndani ya Yanga SC katika mechi zote dhidi ya Medeama ya Ghana Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, wakitoka sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam na kufungwa 3-1 nchini Ghana.

Kwasasa kiungo huyo amepona majeraha yake na anajaribu kurejea kwa ajili ya mchezo ujao Agosti 13 dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Klabu hiyo ilirejea Dar es Salaam Alhamisi usiku ikitokea Ghana ambako Jumanne ilifungwa 3-1 dhidi ya Medeama katika mechi ya Kundi A Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Yanga jana ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wake wa Kaunda, makao makuu ya klabu, Jangwani jijini Dar es Salaam baada ya muda mrefu kutokana na kukosa uwanja wa kukodi kwa ajili ya mazoezi hayo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *