Akaunti mpya ya Instagram inayodaiwa kuwa ya kundi la Destiny’s Child imefunguliwa huku mashabiki wakitumai kwamba huenda kundi hilo limeungana tena.

Akaunti hiyo ambayo imethibitishwa ilionekana siku ya Jumamosi na sasa imechapisha picha za kusherehekea hatua iliopigwa na kundi hilo.

Waimbaji watatu wa kundi hilo walitawanyika mwaka 2006 lakini mwakani kundi hilo itaadhimisha miaka 20.

Hata hivyo mashabiki wameanza kuzua uvumi kuhusu umuhimu wa akaunti hiyo katika siku zijazo.

Akaunti hiyo imefuatwa na takriban mashabiki 12,000 wote wakitaka wanachama wa kundi hilo kufanya ziara ya pamoja.

Wanamuziki wa kundi hilo ni Kelly Rowland,Michelle Williams na Beyonce.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *