Mwanamuziki wa hip hop nhini Marekani, Desiigner amekamatwa na polisi kwa kosa la kukutwa na silaha na dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa mtandaa wa TMZ rapa huyo amekamatwa kutokana na kosa hilo ambalo ni kinyume na sheria za Marekani mtu kumiliki silaha bila vibali pamoja na kukutwa madawa ya kulevya ambayo ni haramu.

Polisi wamesema kuwa rapa na wenzake wanne walikuwa kwenye gari waligombana na dereva mwingine ambaye alipiga simu polisi kuripoti tukio hilo na maafisa wa polisi hao kufika katika eneo la tukio.

Na baada ya polisi kusimamisha gari alilo kuwepo Desiigner walikuta dawa kama OxyContin na kuwakamata vijana wengine wanne.

Desiigner amefunguliwa mashtaka ya kukutwa na dawa za kulevya akiwa na nia ya kuuza pamoja na watu wengine wanne, kosa la kutembea na silaha yenye risasi na kosa la kutishia.

Baada ya kukamatwa kwake kuna kampeni ambayo inaitwa #FreeDesiigner imetumika kama kampeni ya kumtoa jela.

Desiigner ni mwanamuziki aliyejipatia umaarufu duniani kote kupitia ngoma yake ya ‘PANDA’ ambayo inafanya vizuri hadi sasa.

Mwanamuziki huyo yupo chini ya lebo ya G.O.O.D Music iliyochini ya rapa Kanye West ambapo juzi kati lebo hiyo ilimsainisha rapa mwingine, Tyga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *