Golikipa wa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ Denis amesema kuwa atastaafu kuchea soka la kimataifa na kujikita kwenye klabu yake ya Mamelod Sundown.

Kauli ya kipa huyo imekuja siku chache baada ya Timu ya Taifa ya Uganda kutupwa nje ya mashindano ya mataifa ya Afrika mwaka huu.

Onyango ambaye ni mwanasoka bora wa ndani wa Afrika ambaye anacheza Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, amesema anahisi ni muda wa kuwaachia vijana waoneshe uwezo wao kwa Taifa.

Onyango aliiongoza Uganda The Cranes kufuzu michuano ya Mataifa Afrika mwaka huu, na pia ameiongoza katika michezo mitatu ya hatua ya makundi na kupoteza michezo mitatu huku ikiambulia sare ya bao 1-1 katika mchezo wake wa mwisho ilyocheza jana dhidi ya Mali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *