Kiungo wa Tottenham, Dele Alli amefungiwa mechi tatu na shirikisho la soka Ulaya baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu wakati wa mechi dhidi ya timu ya Gent.

Alli alipewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Brecht Dejaegere, timu zote zilipotoka sare ya 2-2.

Iwapo Spurs watafanikiwa kupata tiketi ya moja kwa moja ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao, Alli atakosa nusu ya michuano yao ya makundi.

Spurs, iliyoondolewa katika ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, na Gent.

Kwa sasa ni ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa imebakiza mechi 10.

Alli alikosa hakucheza mechi tatu zilizopita za ligi kuu Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya kumchezea visivyo mwenzake wa West Bromwich Albion Claudio Yacob.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *