Golikipa wa Manchester United, David De Gea ameshinda tuzo ya Golden Glove award katika ligi kuu Uingereza akimshinda golikipa wa Manchester City, Ederson.

Ameshinda tuzo hiyo baada ya mchezo wa jana dhidi ya Westham United uliomalizika O-0 na kumfanya kupata clean sheet ya 18 kwa msimu huu.

De gea amekuwa nguzo muhimu kwa klabu ya Manchester United msimu huu baada ya kusaidai sana kwenye mechi mbali mbali.

Pia kipa huyo ameteuliwa kwenye kikosi cha wachezaji bora wa msimu huu nchini Uingereza kutokana na kiwango chake bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *