Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Kisari Matiku Makori ameapishwa kushika wadhifa huo leo na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akichukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Hamphrey Pole Pole.

Nafasi ya Makori inakuja baada ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, John Pombe Magufuli kumteua Hamphrey Pole Pole kuwa katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM akichuka nafasi ya Nape Nnauye.

Baada ya kumuapisha DC huyo, mkuu wa moa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa wananchi wa Ubungo wanamatumaini na uteuzi wake na lengo kuu la kuanzisha wilaya ya Ubungo ni kusogeza huduma za wananchi karib.

Makonda amemtaka DC huyo mpya kuhakikisha anatatua changamoto za wananchi kwa kuwafuata huko waliko na asiridhike na ripoti anazoletewa ofisini kwani kumekuwepo na changamoto kubwa ya uwajibikaji hivyo inabidi hajiridhishe kwanza mwenyewe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya mpya Makori ameomba ushirikiano kwa viongozi wenzake ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu na kuahidi kuwa atafanya siasa za kuleta maendeleo ili kila mwananchi anufaike na rasilimali zilizopo hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *