Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ameamuru Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) waondoke kwenye maeneo ya wananchi katika eneo lote la Ukonga kuanzia sasa na wasiwabughudhi wananchi.

Mjema amesema hayo leo baada ya kutembelea eneo la Ukonga Mombasa lililokumbwa na vurugu kwa siku mbili baada ya kudaiwa kuuawa kwa askari wa FFU jambo lililofanya askari kupiga watu hovyo na kuzua hofu.

 Amesema wananchi waliojeruhiwa na askari hao wajiorodheshe majina yao na askari waliohusika kuwapiga raia wachukuliwe hatua za kinidhamu kwani hawakupaswa kujichukulia sheria mkononi kama wananchi waliohusika kumuua askari mwenzao.

 Katika eneo hilo hali si salama kwa kuwa maduka na huduma za kijamii zimesimama wananchi wako barabara wakiandamana.

 Mmoja wa wananchi wa eneo hilo, Issa Salehe amesema jana Jumatatu usiku askari wa FFU walivamia eneo lake la biashara wakachukua wakala kisha wakavunja vyombo vyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *