Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw. Andrea Tsere ametoa agizo la kukamatwa kwa wananchi wa kitongoji cha Ngalawale wilayani humo kwa kususia kikao cha mkuu huyo wa wilaya.

Akizungumza katika eneo la tukio mkuu huyo wa wilaya ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha wananchi kususia vikao vya maendeleo vinavyoitishwa na serikali ambapo ikitokea tatizo au mradi ukiwa unafanyika katika eneo lao wanakuwa wa kwanza kulalamika kwamba hawashirikishwi.

Mkuu wa Wilaya amesema “Naagiza wananchi wa kitongoji hiki wakamatwe majumbani hadi walipe faini, haiwezekani tuitishe kikao cha kujadili maendeleo yanayowahusu na wao washindwe kujitokeza hii siyo dalili nzuri katika kuwashirikisha mambo yanayowahusu”.

Aidha tangu ateuliwe kushika wadhifa huo wa ukuu wa wilaya , Bw. Tsere amekuwa akifanya ziara katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi jambo ambalo amesisitiza ushirikiano kutoka kwa wananchi kwani kazi hizo anafanya kwa ajili yao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *