Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi leo anatarajia kuanza ziara ya siku 10 katika kata 10 za wilaya hiyo, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Hapi amesema ziara hiyo ni awamu ya pili baada ya kumalizika awamu ya kwanza iliyozishirikisha kata 10 kati ya 20 zilizopo katika wilaya hiyo.

Amesema lengo la ziara hiyo ni kusikiliza kero za wananchi katika maeneo yao na kuzitafutia ufumbuzi.

Aliongeza kuwa katika ziara hii ya awamu ya pili ataanza kwa kuzungumza na watendaji wa kata na mitaa na baadaye atakwenda katika mkutano wa hadhara kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi.

Hapi alisema ziara itaanzia katika kata ya Mbweni ikifuatiwa na Mzimuni, Kinondoni, Kijitonyama, Wazo, Ndugumbi, Hananasif, Bunju, Mbezi Juu na Makongo Juu.

Ametoa mwito kwa wakazi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi katika mikutano hiyo ili kuja kueleza kero mbalimbali zinazowakabili na namna zitakavyotatuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *