Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi amewapongeza waigizaji wa kike baada ya kujitolea kutoa damu katika hospitali ya Mwananyamala iliyopo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Waigizaji wa kike nchini kupitia chama chao cha Maendeleo CWTF jana waliamua kuchangia damu kwa ajili ya wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

Katika utoaji wa damu huyo kuliamabatana na uzinduzi wa chama chao cha Maendeleo kwa wanawake waigiza CWTF ambapo mkuu wa wilaya huyo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wageni kibao.

Mkuu wa wilaya huyo aliwapongeza wasanii hao kwa kuamua kuunda chama hicho na kuanza na mpango wa kujitolea damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wananchi wenzao ambapo aliwapa pia fursa ya kuandaa tamasha kubwa zaidi ambalo litawafanya wajitangaze zaidi na kuwasihi kujiamini kwani umoja huo ni jambo jema.

Baadhi ya waigizaji hao wa kike waliojitolea damu ni Salome Urassa (Thea),  Nahya Stanslaus (Nina),  Happiness Stanslaus (Nyamayao)  Blandina Chagula ‘Johari’ na  Halima Yahya (Davina).

Picha kwa hisani ya Global Publishers

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *