Mkuu wa Wiliya ya Kinondoni, Ally Hapi ameitaka wizara ya mali asili na utalii kuwatumia wasanii katika kutangaza utalii na vivutio vilivyopo hapa nchini.

Mkuu wa Wilaya huyo amesema kwamba wasanii wanauwezo mkubwa wa kutangaza vivutio mbali mbali hapa nchini kutokana na ukubwa wa majina yao na kuliingizia taifa mapato makubwa na kuboresha maisha yao wenyewe.

Akizungumza na wasanii wa muziki pamoja na filamu bwana Hapi amewataka wasanii kutumia ukubwa wa majina yao katika mitandao ya kijamii kwa kufanya biashara huku akiwahakikishia wasanii hao kuwatafutia walimu wa ujasiliamali.

Pia mkuu wa wilaya huyo amewataka wasanii kujishughulisha katika biashara mbali mbali pia ikiwemo kununua hisa katika makampuni na kuchukua mikopo katika mabenki baada ya kupata elimu ya ujasiliamali.

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *