Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametoa siku 14  kwa uongozi wa soko la Magomeni kuhakikisha wanaondoa baa na ghala vilivyopo katikati ya soko hilo.

Akizungumza katika ziara yake ya siku 10 ndani ya wilaya hiyo, Hapi alisema inasikitisha kuona hata wamiliki wa ghala hizo hawafahamiki.

Amesema uwepo wa ghala na baa katikati ya soko hilo inawanyima fursa wafanyabiashara walio wengi hasa wafanyabiashara wadogo.

Ameongeza kwa kusema ‘Ninatoa siku 14 kwa viongozi wa soko na manispaa kuhakikisha wanaaondoa maghala haya kwani inaonyesha ni ya wafanyabiashara wakubwa hivyo waende kwa wenzao hapa hapawafai’.

Sambamba na hilo mkuu huyo wa wilaya ametoa siku 14 nyingine kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya soko hilo kurejea ndani ya soko.

Pia amesema ‘Hakuna aliyeruhusu wafanyabiashara wengine kufanyabiashara nje ya soko hivyo naagiza ndani ya siku 14 wote mhamie ndani kwa sababu mnaleta usumbufu kwa wengine na kuleta malalamiko’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *