Mwanamuzki mkongwe wa Bongo fleva, Daz Baba amekanusha taarifa zinazoenea mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatumia dawa za kulevya na ndiyo sababu ya kupotea kwenye muziki huo.

Daz Baba amesema kwamba wanamchafua sana na vil e vile hakuna lolote wanalomsaidia zaidi ya kumsema vibaya katika mitandao ya kijamii na waadau wa muziki wanashindwa hata kumsaidia kwa kumtafutia hata show yeyote.

Staa huyo ameongeza kwa kusema muda wote amekuwa nyumbani kwao akisimamia familia yao baada ya baba yake mzazi kuuawa, jambo ambalo amesema aliwezi kufanywa na mtu anayetumia madawa ya kulevya.

Pia Daz Baba amesema huwa aonekani sana katika sehemu mbali mbali kama ilivyo kwa wasanii wengine kutokana na kuzushiwa mambo yasiyofaa na yakumvuruga.

Daz Baba au Daz Mwalimu ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wanaunda kundi la Daz Nundaz Family lililojizolea umaarufu kupitia nyimbo zake za kuuzunisha kama vile Kamanda, Barua na Maji ya shingo, wasanii wengine waliokuwa wanaunda kundi hilo ni Ferooz, Sajo, Lalumba na Scout Jenta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *