Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dayna Nyange amekuwa mtanzania pekee aliyechaguliwa kuwania tuzo za BAE Awards 2017zitakazofanyika nchini Nigeria.

Dayna Nyange amechaguliwa katika vipengele viwili BEST AFRICAN ACT akichuana na Eddy Kenzo (Uganda), King Kaka (Kenya), Stoneboy (Ghana) pamoja na Jah Vinci (Jamaica).

nyange

Pia amechaguliwa kuwania Kipengele cha BEST VOCAL PERFORMANCE FEMALE kupitia wimbo wake ‘Angejua’ ambapo anawania tuzo hiyo na Aramide, Ngowari na Rocknana (wote kutoka Nigeria).

Ni kwa mara ya kwanza masanii huyo kuchaguliwa kuwaniwa tuzo za kiamataifa baada ya kupata nafasi kwenye tuzo hizo nchini Nigeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *