Dayna Nyange kuachia ngoma na Patoranking

0
248

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dayna Nyange amefunguka na kusema kuwa yuko kwenye maandalizi ya kuachia nyimbo mpya akiwa na mwanamuziki wa Nigeria Patoranking.

Dayna amewahi kutamba na ngoma kali kama vile Angejua, Komela akiwa na Billnass na Nivute Kwako aliyomshirikisha Barnaba.

Dayna alisema mashabiki wake wakae mkao wa kula kutokana na ‘project’ kali zinazotarajia kushuka hivi karibuni.

“Nimekuwa kwenye ziara yangu binafsi hapa Nigeria ambayo imekuwa na lengo la kujifunza kwa kujionea wenzetu wanafanya nini katika kiwanda cha muziki ambacho kinawafanya wazidi kufanikiwa.

“Pamoja na hayo kulikuwa na plani ya kufahamiana na mastaa wa Nigeria ambao tumekuwa tukiwasiliana tu bila kuonana, na nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika hilo kwani nimeweza kukutana na Patoranking, D’banj na meneja wa Wizkid.

“Patoranking ni mtu poa na kuna vitu vingi ambavyo tumefanya pamoja vinakuja ila nisingependa kusema mengi kwa sasa bali wakati utakapofika mashabiki wangu watajua kitu gani kinafuata.

LEAVE A REPLY