Mwanamitindo wa Tanzania, Daxx Cruz ametaja vigezo vya mtu anayestahili kuwa mwanamitindo na kutaja baadhi ya wanamitindo wa Tanzania wasiokuwa na vigezo.

Daxx ambaye kwasasa shughuli zake anazifanyia nchini Afrika Kusini amemtaja model anayefahamika kwa jina la Calisah kuwa hastahili kabisa kufanya kazi hiyo kwa kuwa hana vigezo.

Mwanamitindo huyo amemtaja Hamisa Mobeto kuwa hastahili kuwa ‘model’ kwa kuwa amekaa kiurembo zaidi na kwamba anafaa kwa kazi ya kuonekana kwenye video za miziki (Video Vixing) hivyo kutokidhi vigezo vya kimataifa vya kuwa ‘model’ labda kwa Tanzania.

Amewataja baadhi ya watu ambao anadhani kuwa ni ‘models’ wazuri na ambao endapo watakaza, watafika mbali kuwa ni pamoja na Nelly Kamwelu.

Pia Daxx ametaja model watatu wa kike ambao anawakubali zaidi Bongo na anaona ni pesa sehemu yoyote watakapokwenda kuwa ni pamoja na Alexia, Zuhua Goa na Batuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *