Mwanamitindo wa Tanzania ambae anaishi  na kufanya kazi zake nchini Afrika ya Kusini, Daxx Cruz amemchana Calisah kwa kitendo chake cha kuvaa viatu vya kike.

Daxx Cruz amesema kuwa kitendo icho cha mwanamitindo huyo kufanya kazi za kike ni kuiaibisha tasnia hiyo.

Calisah wiki chache zilizopita alifanya kazi ya kupiga picha akifanya matangazo ya viatu vya kike japokuwa yeye ni mwanaume.

Baada ya kuzagaa kwa picha hizo katika mtandao baadhi ya watu walianza kumsema na kukashifu kitendo icho kuwa ni tabia mbaya .

Kwa upande wake calisah mwenyewe hakuonekana kujali baadhi ya maneno ya watu katika mitandao badala yake alisema kuwa yeye ana uwezo wa kufanya kazi zote ilimradi tu kazi iyo iweze kumlipa ela itakayo msaidia kumudu maisha yake.

Daxx Cruz amesema kuwa hata yeye yupo katika tasnia hiyo ya modelling kwa muda mrefu lakini hawezi kufikia hatua ya kufanya kazi kama hizo kwa sababu ni kazi ya kike na wapo models wa kike na kwa mwanaume aliekamilika hawezi kufanya kitendo kama hicho ambacho hajawahi kuona kimetokea  Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *