Mwanariadha wa Kenya, Rita Jeptoo ameongezewa kifungo cha miaka miwili kutoshiriki mchezo huo kutokana na tuhuma za kutumia dawa za kusisimua misuli.

Uamuzi huo umepitishwa na mahakama ya kutatua mzozo katika michezo Switzerland, unazima matumaini kwa mwanariadha huyo kurudi mchezoni katika miaka ya hivi karibuni.

Mshindi huyo wa mara tatu wa mbio za Boston marathon ameshindwa katika rufaa aliyokata kupinga kuongezwa muda wa miaka hiyo miwili uliokuwa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Wito wa kuongeza marufuku hiyo ulitolewa katika kesi dhidi yake na shirikisho la kimataifa la riadha IAAF.

Rita Jeptoo amepatikana na hatia ya kutumia dawa hizo za kusisimua misuli na shirikisho la riadha Kenya katika uchunguzi aliyofanyiwa mnamo 2014: alipatikana kutumia dawa ya kushinikiza damu EPO.

Matokeo yake katika mashindano tangu Aprili mwaka huu yamefutiliwa mbali ikiwemo ushindi wake katika mashindano ya Boston na Chicago marathon alikoibuka nambari moja.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *