Baada ya kimya cha muda mrefu mwanamuziki nyota wa Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ amesema kuwa anatarajia kuachia nyimbo yake mpya inayoitwa kwa jina la ‘How Long’ kesho siku ya Ijumaa.

Davido amekuwa kimya kwa muda mrefu mpaka kupelekea kutokuwepo kwenye tuzo za MTV MAMA Afrika zitakazofanyika jijini Johannesburg nchini Afrika kusini Oktoba 22 mwaka huu.

Hapo nyuma kulikuwa na marumbano kati ya Davido na kampuni yake inayommliki ya Sony ambayo inadaiwa ndiyo chanzo cha Davido kukaa kimya bila ya kutoa nyimbo kutokana na kutoelewana miongoni mwao.

Ni muda mrefu msanii huyo amekuwa kimya lakini kwa sasa ameonekana kuanza kuachia kazi zake kwa kasi ikiwa ni siku chache zimepita tangu alipoachia wimbo wake mpya pamoja na video ya ‘Gbagbe Oshi.’

Davido anatarajiwa kuachia video ya wimbo wake mpya ‘How Long’ aliomshirikisha msanii kutoka Marekani, Tinashe lakini pia wimbo huo unapatikana kwenye albamu yake mpya, Son of Mercy.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *