Mwanamuziki nyota wa Nigeria, Davido kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha kwamba anatarajia kuachia albamu yake mpya mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Albamu hiyo inajumla ya nyimbo 10 amabayo ameipa jina la ‘Son of Mercy’.

Davido kupitia ukurasa wake wa Instagrama ameandika kama ifuatavyo, “SEPTEMBER WE BEGIN THE JOURNEY TO THE ‘SON OF MERCY’ DOUBLE E.P !!!.”

Albam hiyo itakuwa ni ya tano kwa Davido kwani tayari ameshaachia albamu nne ikiwemo ‘Omo Baba Olow’, ‘The Baddest’, ‘Gobe’ na ‘Best Of Davido’.

Januari mwaka huu msanii huyo amesaini dili na kampuni ya Sony Music kwa ajili ya kusimamia kazi zake zote za muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *