Mkali wa muziki kutoka Nigeria, David Adeleke amesema kuwa anatarajia kurudi chuoni kusoma ili kuweza kujiimarisha zaidi kieleimu.

Davido ameseema kuwa atajiunga na Chuo Kikuu cha Babcock kusoma Shahada ya Udhamili ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) ili aweze kujiweka sawa kielimu.

Staa huyo anatazamiwa kujipanga na kujiandaa kupambana vilivyo baada ya kushuka kimuziki hivi karibuni kutokana na kukaa kimya kwa kipindi kirefu.

Davido ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘How Long’ aliyemshirikisha mwanamuziki Tinashe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *