Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, David Adeleke maarufu kama Davido amesaini mkataba mwingine na label ya RCA Records kutoka nchini Marekani ambapo itakuwa ikisimamia kazi zake zote za muziki.

Licha ya kusaini mktaba huo, Davido bado anaendelea na mkataba wake na kampuni ya Sony Music Global aliosaini mapema mwezi Januari mwaka huu.

RCA Records ni rekodi maarufu nchini Marekani ambapo inawasimamia wasanii wakubwa wakiwemo ASAP Ferg, ASAP Rocky, Alicia Keys, Aretha Franklin, Zayn Malik, Usher, T-Pain, Shakira, Justin Timberlake na Pink.

Davido ambaye kwasasa muziki wake umetanuka baada ya kufanya kazi mbali mbali na wanamuziki tofauti nchini Marekani na kumuwezesha kuchukua tuzo tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *