Mwanamuziki nyota wa Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ amewaomba Wanigeria kumpa muda rais, Muhammadu Buhari kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili nchi hiyo.

Davido amesema wananchi wa Nigeria wanatakiwa wampe muda rais huyo ili aweze kuirejesha nchi sehemu nzuri kama ilivyokuwa apo awali na hawapaswi kumlamu kama wanavyofanya.

Buhari: Rais wa Nigeria
Buhari: Rais wa Nigeria

Davido amesema anaamini rais huyo ni kiongozi mzuri lakini anahitaji muda kuiweka nchi sehemu nzuri kiuchumi.

Nigeria kwa sasa inakabiliwa na hali ngumu ikidaiwa kuwa uchumi wake umeshuka na kusababisha mzunguko wa fedha kuwa mdogo jambo mpaka kupelekea kumpa lawama rais Buhari.

Davido ni mwanamuziki ambaye anafanya vizuri katika medani ya muziki nchini Nigeria ameamua kumkingia kifua rais huyo baada ya wananchini kutokuwa na imani naye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *