Mwanamuziki wa Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ amelazwa hospitali kutokana na kusumbuliwa na mawazo ‘stress’.

 Davido amekuwa akisumbuliwa na skendo inayozidi kuenea kwa kasi kuhusiana na kuzaa na mwanamke anayefahamika kama Ayomide Labinjo.

Mwanamuziki huyo aliweka video kwenye mtandao wa Snaptchat akiwa ametundukiwa dripu na kuwaambia mashabiki wake wamuombee.

Hivi karibuni, Ayomide alizungumza na Jarida la Punch na kuanika kila kitu kuwa, amezaa na Davido baada ya kulazimishwa wasitumie kinga.

Ayomide kwa kushirikiana na mama yake wameshafungua mashtaka yakumtaka Davido ashiriki katika malezi ya mtoto huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *