Staa wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ amesema kwamba ameingia rasmi katika mpango wa kuwasomesha wanafunzi nchini humo ili waweze kujikwamua kimaisha.

Mwanamuziki huyo baba yake naye alishawahi kusomesha wanafunzi 200 miaka ya nyuma, amesema mipango yake ni kusomesha wanafunzi kupitia mradi maalum wa mama yake, Veronica.

Davido amesema mwaka huu ataanza kusomesha wanafunzi kupitia mradi wa mama yake unaoitwa Veronica Education Scholarship Program.

Vile vile staa huyo amesema kwamba atakuwa anawasomesha wanafunzi bure kila mwaka ambapo mwaka huu ataanza na wanafunzi wanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *