Mwanamuziki nyota wa Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ anachunguzwa na Polisi nchini humo kufuatia kifo cha rafiki yake wa karibu anayeitwa kwa jina la Tagbo Umeike.

Polisi katika mji wa Lagos nchini Nigeria wamesema kuwa wanamchunguzua mwanamuziki huyo kufuatia utata unaozunguka kifo cha rafiki yake.

Msemaji wa polisi nchini humo amesema kuwa Davido hakuchukuliwa kuwa mshukiwa ila aliitwa kuhojiwa pamoja na familia ya Tagbo ambao walikuwepo wakati wa kifo chake.

Polisi hao wamesema kuwa wanachunguza ili kupata picha wazi kuhusu kile kilichotokea. alisema msemaji huyo.

Tagbo ambaye ni rafiki yake Davido alifariki tarehe 3 Oktoba mwaka huu na mwili wake ukaachwa nje ya hospitali mjini Lagos nchini Nigeria.

Baada ya kufanyiwa mahojiano hayo, Davido amekana kabisa kuhusika kwenye kifo cha rafiki yake huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *