Mwanamuziki nyota kutoka Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ amefurahishwa baada ya nyimbo yake ‘Skelewu’ kutimika katika movie mpya ya Hollywood inayoitwa ‘Queen of Katwe’.

 Kupitia mtandao wake wa Twitter Davido amefunguka namna ambavyo ameshangazwa na kufurahishwa kusikia nyimbo yake imechaguliwa kutumika kwenye movie hiyo mpya itakayotoka mwaka huu.

Queen of Katwe: Kipande cha movie hiyo mpya.
Queen of Katwe: Kipande cha movie hiyo mpya.

Movie hiyo (Queen of Katwe) ambayo amecheza Lupita N’yongo na David Oyelowo kama wahusika wakuu.

Movie hiyo ambayo Lupita pamoja na David Oyelewo wameanza kuipiga promo itatoka rasmi Septemba 23 kwenye majumba ya sinema.

Skelewu ni nyimbo ambayo ilimpa umaarufu Davido mpaka kupelekea kufahamika Afrika kutokana na nyimbo hiyo kuenenea Afrika nzima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *